Latest Posts

LIMENI KWA TIJA KUIMARISHA MAPATO YA HALMASHAURI – MALIMA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema kuwa mapinduzi ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kumechangia kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato ndani ya Halmashauri hiyo.

Malima amesema hayo Julai 9, 2026 wakati akifungua kikao maalum cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali [CAG] kilichofanyika Wilayani humo.

Amesema mazao yanayoweza kuongeza mapato hayo yakilimwa kwa wingi ni pamoja na viazi mviringo na tumbaku ambapo viazi vitatumika kwa walaji wa chips na tumbaku kuuzwa katika kiwanda ambacho kipo Mkoani Morogoro.

Kwaa sababu hiyo mazao hayo yanatakiwa kulimwa kwa tija ili kuongeza thamani na hivyo kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo sambamba na kulima zao la jamii ya mikunde.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka madiwani kusimamia miradi ya maendeleo na kufanya kazi kulingana na nafasi zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha huduma kw jamii na kukaamilisha kwa wakati miradi y maendeleo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa ameipongeza halmashauri kwa juhudi ya kuongeza ukusanyaji mapato huku akibainish kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya mapato kiasi cha shilingi Bilioni 2 ambapo miaka miwili iliyopita halmashauri ilikuwa na uwezo wa kukusanya Sh. Mil. 800 pekee.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo Ramadhan Kimwaga akifunga kikao hicho amekiri kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na ya kikao hicho kuyafanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!