Latest Posts

NYANGE AFICHUA MIKAKATI ILIYOIWEZESHA MTWARA MIKINDANI KUSHIKA NAFASI YA 8 KITAIFA

Manispaa ya Mtwara Mikindani imefanikiwa kushika nafasi ya nane kitaifa kati ya halmashauri 184 katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (NECTA) 2025, mafanikio ambayo yameelezwa kuchangiwa na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi.

Akizungumza na walimu wa shule za sekondari na msingi pamoja na wakuu wa idara wa manispaa hiyo katika Shule ya Sekondari Tandika kwa lengo la kuwapongeza, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange, amesema miongoni mwa mikakati iliyotekelezwa ni kuwaweka kambini wanafunzi 105 kutoka shule mbalimbali waliopata daraja la nne na sifuri katika mtihani wa moko, hatua iliyolenga kutokomeza sifuri katika halmashauri hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Elimu wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mwalimu Mangula Mayemba, amesema wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanadumisha nafasi hiyo au kupanda juu zaidi katika matokeo yajayo ya mitihani ya taifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!