Latest Posts

DC AAGIZA WANAODANGANYA KUHUSU MAFUNZO YA MGAMBO WAKAMATWE

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Juma Sweda ameagiza kukamatwa viongozi au mtu yeyote anayewadanganya vijana juu ya mafunzo ya mgambo na kuwafanya watoroke mafunzo hayo.

DC Sweda ametoa agizo hilo wakati akizungumza na vijana waliojiunga na mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) katika kata ya Utalingolo halmashauri ya mji wa Njombe.

“Nimeshangaa vijiji vingine hawajaja, waambieni waje ni lazima wala sio hiari kama kuna mtu anawadanganya awe ni mwenyekiti wa kitongoji kamata weka ndani”, amesema DC Sweda

Awali Diwani wa kata ya Utalingolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmshauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema kuna umuhimu mkubwa wa mafunzo hayo ikiwemo kulinda usalama kwenye maeneo yao huku Aladini Kamaru mashauri wa mgambo wilaya ya Njombe akibainisha kuwa mpaka sasa vijana zaidi ya 100 wamejiunga na mafunzo katika kata hiyo.

Wakazi wa Utalingolo akiwemo Omben Mabena wametoa wito kwa vijana waliokimbia mafunzo kurejea ili pia waweze kuimarisha afya zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!