Latest Posts

KHAMENEI AZIKWA, МОЈТАВА ВADO HAJAONEKANA HADHARANI

Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amezikwa katika eneo takatifu la Shrine ya Imam Reza mjini Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran, huku mwanawe na mrithi wake, Mojtaba Khamenei, akiendelea kutoonekana hadharani tangu kutangazwa kuwa kiongozi mpya wa juu wa nchi hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Mojtaba Khamenei bado anaendelea kupona majeraha aliyoyapata katika shambulio lililomuua baba yake, huku hatua kali za kiusalama zikichukuliwa kuzuia kuonekana kwake hadharani kwa hofu ya mashambulizi zaidi.

Mazishi ya Khamenei yamehitimisha wiki moja ya shughuli za maombolezo zilizofanyika nchini Iran na Iraq, zikiwemo misafara ya mazishi, ibada na mikusanyiko ya wananchi.

Mwili wake ulisafirishwa kupitia mitaa ya Mashhad iliyokuwa imejaa waombolezaji waliobeba bendera za Iran, picha zake na mabango yenye ujumbe wa mapinduzi, huku viongozi wa kidini wakiongoza taratibu za mwisho za mazishi.

Khamenei aliuawa Februari 28, 2026, katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani na Israel mwanzoni mwa vita vilivyodumu kwa miezi minne, kabla ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi uliopita.

Wakati wa mazishi hayo, baadhi ya waombolezaji walitoa kauli kali dhidi ya Marekani na Rais Donald Trump, wakitaka kulipiza kisasi kwa kifo cha Khamenei.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!