Na Helena Magabe Mwanza .
Kumekuwepo na malalamiko kwa Wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na migodi Kanda ya ziwa wakidai kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira kunakohatarisha afya zao hatua iliyopelekea Jambo tv kufika katika Ofisi za baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC)Kanda ya ziwa ili kupata ufafanuzi.
Kaimu Meneja wa Baraza la usimamizi wa mazingira Ofisi za kanda ya mashariki inayohusisha Mikoa mitatu ambayo ni Mara, Simiyu na Mwaza , Boniphace Chacha amesema hivi karibuni walifanya ukaguzi kwenye migodi iliyopo Mkoa wa Mara na kubaini makosa mbali mbali ikiwemo utiririshaji wa maji yaliyochanganyikana na kemikali kuingia kwenye mazingira licha ya kuwa kifungu cha 4 cha sheria ya mazingira kinasema kila Mtu ana haki ya kuishi mazingira safi na salama.
Chacha amesema walibaini pia kuwepo kwa Wafanyabiashara wa uchimbaji wa madini kutokuwa na vibali vinavyotolewa na NEMC kwaajili ya kufanya shughuli hiyo,ukiuwakwaji wa masharti ya kwa wale waliopewa vibali na vile vile kuwepo kwa utunzaji wa taka usio sahihi na hasa taka hatarishi ambapo walichukua hatua kwa  kuwatoza faini wasio na vibali ambapo faini huwa ni milioni tano 5,000,000   kwa makosa  mbali mbali kwa mujibu wa sheria No:20 ya mazingira ya mwaka 2024 .
Aidha amesema kuanzia julai 13 ,2026 wiki ijayo wataanza ukaguzi kwenye migodi iliyopo kwenye Wilaya zote zilizopo Mkoa wa Mwanza ambapo zoezi litafanyika hadi Agosti likifatiwa na Mara ambapo zoezi litafanyika katika Wilaya zote hadi Septemba huku Simiyu likifatia hadi mwezi wa Octoba ambapo kwa kutoa elimu na ushauri na baada ya miezi mitatu hiyo wataendelea kufanya ukaguguzi,
Mbali na hayo katika ukaguzi huo walibaini kuwepo kwa uhaba wa vitendea kazi ambavya ni vifaa kinga ambapo alisema
Wataendelea kushirikiqna na wadau wengine kuhakikisha hakuna uchafuzi wa vyanzo vya maji pamoja na mazingira na watakaobaika watachukuliwa hatua.
Mwisho.