Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali ya Tanzania kutoa haki ya ardhi kwa wananchi wa Ngorongoro kama ilivyo kwa Watanzania wengine.
Hayo yamesemwa na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo Jijini Dar es Salaam.
Semu ametoa wito kwa Serikali kubatilisha tangazo haramu la namba 673 la mwaka 2024, linalopendekeza kufuta vijiji vya Ngorongoro na maeneo mengine nchini, na majina yaliyondolewa kwenye daftari la wapiga kura kurejeshwa.
Aidha, Semu amesisitiza kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ivunjwe na iundwe kampuni yenye ushiriki na umiliki wa ubia kati ya Serikali na wananchi wa Ngorongoro kama suluhisho la mgogoro wa ardhi.