Latest Posts

ACT WAZALENDO YALIA NA WACHIMBAJI WADOGO KYERWA

 

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu ameitaka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) kutekeleza ahadi yake ya kupeleka vipimo vya kubaini kiwango cha madini ya bati Wilayani Kyerwa ili kuwaepusha wachimbaji wadogo na unyonyaji kwenye mauzo.

Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu ametoa rai hiyo alipotembelea mgodi wa madini ya tin (bati) uliopo katika Kijiji cha Nyaruzumbura Wilayani Kyerwa Mkoa wa Kagera.

“Nimejulishwa kuwa kwa utaratibu, bei ya madini ya bati inategemea kiwango cha madini hayo kwenye jiwe jambo linalohitaji vipimo maalum kubaini. GST iwajibike kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili kuhakikisha madini hayo yanawapa tija wachimbaji”- alisisitiza Ado Shaibu.

Katika hatua nyingine, Ndugu Ado ameitaka GST kufanya utafiti wa kina kubaini maeneo yenye madini ya bati katika Mkoa wa Kagera ili kuvutia wawekezaji. Pia, aliitaka Serikali, kupitia Wizara ya Madini, kuwawezesha wachimbaji wadogowadogo wa madini ya bati Wilayani Kyerwa kupata maeneo ya kuchimba madini hayo na pia kuboresha miundombinu katika migodi, hasa upatikanaji wa huduma ya uhakika wa huduma za maji na afya.

“Nchi kote, wachimbaji, hasa wachimbaji wadogowadogo wana changamoto kubwa. Lakini, wachimbaji wa madini ya bati wamesahaulika zaidi. Nimetembelea hapa mgodini ili kutuma ujumbe kuwa ACT Wazalendo ipo tayari kuwa sauti ya Wachimbaji wadogowadogo nchini” alisisitiza Shaibu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!