Latest Posts

ACT YAONYA KUHUSU MPASUKO WA KITAIFA MAADHIMISHO YA CHADEMA KUINGILIWA NA POLISI

Sakata la kuzuiliwa kwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 33 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Rukwa limechukua sura mpya baada ya chama cha ACT Wazalendo kuingilia kati na kulaani kile walichokiita uonevu na ukandamizaji dhidi ya CHADEMA.

Madai ya kuzuiliwa kwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 33 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Rukwa yamechukua sura mpya baada ya chama cha ACT Wazalendo kuingilia kati na kulaani kile walichokiita uonevu na ukandamizaji.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Januari 22, 2026, na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa ACT, Shangwe Ayo, chama hicho kimeelezea kusikitishwa na hatua ya Jeshi la Polisi wilayani Nkasi kuzuia shughuli za kijamii za CHADEMA, ikiwemo upandaji miti, zilizopangwa kufanyika Januari 21.

“Shughuli za kijamii kama upandaji wa miti ni shughuli zinazopaswa kupongezwa na kuungwa mkono kutokana na umuhimu wake katika kutunza na kihifadhi mazingira. Inapotokea taasisi au watu wanaojitolea kufanya shughuli za namna hiyo, ambazo zinalenga kutoa mchango katika kutatua changamoto zinazolikabili taifa halafu wakazuiwa wasifanye, tafsiri yake ni kwamba Serikali sasa inataka nchi yetu iendelee kusalia na changamoto hizo. Tunajiuliza, hiyo ni kwa manufaa ya nani, hakika hatupati majibu!”, ameeleza Shangwe.

ACT Wazalendo imedai kuwa kitendo hicho ni mwendelezo wa vitendo vya kudhoofisha demokrasia na vyama vya upinzani. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, ingawa kuna zuio la muda la mahakama kwa CHADEMA kufanya mikutano ya kisiasa, zuio hilo halihusiani na shughuli za kijamii zenye manufaa kwa taifa kama utunzaji wa mazingira.

“Tunakitazama na kukitafsiri kitendo cha kuzuiwa CHADEMA kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kuwa cha uonevu, ukandamizaji na kikatili. Ni kitendo cha kishenzi kisichokuwa cha kiungwana katika nchi yetu. Ni kitendo kibaya kinachochea chuki, mpasuko na mgawanyiko wa kitaifa. Ni kitendo kinachorejesha nyuma jitihada zetu kama taifa za kujenga umoja, upendo, amani na mshikamano wetu kama Watanzania. Ni mwendelezo wa kukandamiza uhuru wa raia, demokrasia na vyama vya upinzani nchini”, imeelezwa katika taarifa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa lilikanusha vikali taarifa zilizombatana na taarifa ya zuio hilo za uvamizi wa nguvu, kutawanya na kukamatwa kwa Wanachadema wakati wa zoezi la upandaji miti likiziita ni upotoshaji wenye lengo la kuzua taharuki. Katika taarifa yake, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo alisisitiza kuwa hakuna mwanachama wa CHADEMA aliwataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa mitandaoni, wakidai kuwa hali ya usalama mkoani Rukwa ni shwari na hakuna tukio lolote la matumizi ya mabavu lililotokea.

Taarifa ya Polisi ilikuja baada ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, kuandika kupitia mtandao wa X kuwa wafuasi wa chama chake walivamiwa na kukamatwa wakati wakitekeleza zoezi la kupanda miti ofisini kwao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!