Latest Posts

ADC: KUKAMATWA KWA LISSU NI FEDHEHA KWA TAIFA

Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimelaani vikali kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, huku kikitoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kuhakikisha anaachiwa huru mara moja.

Akizungumza na Jambo TV, Mwenyekiti wa ADC Taifa, Shaban Itutu, amesema kitendo cha kumkamata Lissu kama mhalifu wa kawaida ni fedheha kwa taifa, viongozi wa serikali na Jeshi la Polisi.

“Nimuombe Rais aingilie kati suala hili na wamwachie Lissu mara moja ili aweze kuendelea na shughuli zake za kisiasa. Kwa sababu mimi sijaona kosa lake kwenye No Reform No Election, yupo ndani ya haki zake za kikatiba na kisheria,” amesema Itutu.

Aidha, Itutu amelionya Jeshi la Polisi kuacha kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa na badala yake lijikite katika kazi yake ya msingi ya kulinda amani na usalama wa nchi.

“Polisi sio wanasiasa. Wao wanapaswa kulinda amani ya nchi, sio kuzima mikutano ya vyama au kukandamiza haki ya kukosoa. Wanalipwa kupitia kodi za Watanzania kwa kazi ya kulinda usalama, siyo kushindana na vyama vya siasa,” ameongeza.

Itutu pia ameonesha kusikitishwa na uamuzi wa polisi kumfungulia Lissu kesi ya uhaini kesi ambayo ni ngumu kupata dhamana akisema kuwa kuna uwezekanot taifa la Tanzania likampata Rais ambaye anatoka gerezani.

“Hii si hadithi mpya. Zambia iliwahi kupitia hali kama hii, na leo nchi hiyo inaongozwa na Rais aliyepitia mateso kama haya,” amesema.

Mwisho, Itutu amewataka polisi kuonesha uvumilivu na hekima wakati huu wa kuelekea kampeni na uchaguzi, akisisitiza kuwa huu ni wakati wa vyama vya siasa kutimiza majukumu yao ya kidemokrasia bila hofu wala bugudha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma iliyotolewa siku moja baada kuripotiwa kukamatwa kwa Lissu, Lissu alikamatwa kutoa matamshi ambayo yanaweza kuashiria uvunjifu wa amani na kuyumbisha utaratibu wa kikatiba wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu kama inavyotarajiwa na Watanzania.

Jeshi la Polisi lilitoa onyo kwa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa ujumla kuepuka kauli au matendo yanayoweza kusababisha taharuki na kuharibu amani, likisisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayekiuka sheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!