Latest Posts

AFUNGWA MAISHA BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

Mahakama Kuu kanda ya Iringa imemhukumu kifungo cha maisha jela Rashid Mwasema (37) baada ya kumkuta na hatia ya kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin pipi 58 zilizokuwa na kilo 1.01 na dawa hizo zilikuwa tumboni.

Mwasema alikamatwa Machi 31, 2023 alipokwenda kutibiwa katika kituo cha afya cha Mtandika baada ya kuhisi maumivu ya tumbo na baadaye alisema ukweli na kutolewa dawa hizo kwa njia ya haja kubwa.

Rashid Mwasema alikuwa akisafirisha dawa hizo akitokea nchini Msumbiji kupitia Tunduma, na alipofika eneo la Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo alishuka na kuelekea katika Kituo cha Afya cha Mtandika kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya.

Baada ya taratibu za kumpima akalazimika kusema ukweli kuwa alikuwa amebeba dawa za kulevya tumboni ndipo taarifa zikatolewa kwa Jeshi la Polisi na baadaye taratibu za kutoa pipi hizo zipatazo 58 zikafanyika.

Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 11 akiwamo Daktari aliyesimamia kutolewa kwa pipi hizo, Mkemia Mkuu alithibitisha kuwa pipi hizo ni dawa za kulevya aina ya Heroin pamoja na Jeshi la Polisi waliohusika katika kumkamata.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Ilvin Mgeta amesema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo Rashid Mwasema amekutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya na adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Kesi hiyo ilikuwa na waendesha mashitaka wa serikali Magreth Mahundi na Yahya Misango ambao waliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo kwa sababu dawa za kulevya zinaharibu vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake Wakili wa utetezi aliomba mahakama kumpunguzia mteja wake adhabu kwa sababu ni kosa lake la kwanza na afya ya mteja wake siyo nzuri. Hata hivyo Mahakama ikamhukumu adhabu kifungo cha maisha jela Rashid Mwasemwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin pipi 58 zilizokuwa na uzito wa Kg 1.1

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!