Latest Posts

AKINA MAMA WATAKIWA KUJENGA UKARIBU NA WATOTO WAO ILI KUWALINDA DHIDI YA UKATILI

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Rebeka Nsemwa amewasihi akina mama kusimama imara katika malezi ya watoto kwa kujenga ukaribu na vijana wao katika kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili.

Nsemwa ametoa nasaha hizo wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanawake wapambanaji katika biashara, uongozi na uwajibikaji kwa jamii, zinazoandaliwa na Taasisi ya Ladies Talk Tanzania mkoani Morogoro, ambapo amesema familia yenye ustawi mzuri wa malezi ndiyo inayozalisha Taifa lililo bora kwa kesho.

Amesema kwa ustawi wa Taifa lililo bora kunahitajika wanawake wenye ushupavu, ujasiri na uthubutu.

“Niwasihi muda mwingi mnaotumia kutafuta mali kumbukeni na wajibu wenu wa malezi” Amesema  Nsemwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Taasisi ya ladies Talk Tanzania Salome Sengo amesema Taasisi hiyo imeandaa tuzo hizo kwa lengo la kuwatambua wanawake katika sekta mbalimbali, pamoja na kuwajengea uwezo wa kuinuka kiuchumi kupitia shughuli wanazofanya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!