Latest Posts

AMOSI- CCM ITAENDELEA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA WANANCHI

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni Mlezi wa Kata ya Hananasif, Amosi Simon Richard akiwa ameambatana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya Andrew Gesungura tarehe 20 Novemba, 2024 amezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mitaa 5 Kata ya Hananasif, amesema kuwa CCM itaendelea kuwa chachu ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa Hananasif.

Amesisitiza muhimu wa Wananchi wa Hananasif kuchagua wagombea wa CCM kwani ni waadilifu, wanajali maslahi ya wananchi, wanafikika, wana uzoefu wa uongozi na uwezo wa kutatua changamoto za kijamii kwa ufanisi mkubwa.

“Ndugu Wananchi CCM imejenga msingi imara wa utawala bora, na viongozi wake wanajali maslahi ya wananchi. Kuchagua viongozi wa CCM ni kuchagua uongozi wa kuleta maendeleo katika Mitaa yetu, usalama, huduma bora kwa wananchi na kutunza amani yetu.” Amesema.

Aidha Amosi amekumbusha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinajivunia historia yake ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayohusiana na sekta za afya, elimu, miundombinu, na huduma za jamii, ambazo zimeleta mabadiliko chanya kwa wananchi katika Mitaa ya Kata hiyo tangu nchi yetu ilipopata Uhuru 1961.

Uzinduzi wa kampeni hizo pia uliambatana na utambulisho wa wagombea nafasi za uenyekiti wa Mitaa ya Kawawa, Mkunguni A, Mkunguni B, Kisutu na Hananasif pamoja na wagombea wa nafasi za ujumbe, ambapo walijitambulisha kwa wananchi, kuomba kura na kuahidi kutekeleza ahadi za maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote.

Mwisho, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni ametoa wito kwa vijana na wananchi wa Kata ya Hananasif kujitokeza kwa wingi na kuwachagua viongozi wa CCM, ili kuendeleza chachu ya maendeleo na mapinduzi ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa kwa manufaa ya kila mwananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!