Latest Posts

ASKOFU BAGONZA AHOJI UWAZI WA KESI YA UHAINI: “UJINGA WANGU SASA UMEKOMAA”

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ameibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha ujumbe wa tafakari nzito uliojaa maswali ya msingi kuhusu uwazi wa kesi ya uhaini inayomkabili mtuhumiwa mmoja nchini.

Kupitia chapisho lenye kichwa kinachosema “Ujinga Wangu Sasa Umekomaa”, Askofu Bagonza amesema alikuwa anaamini kuwa kosa la uhaini ni jambo kubwa linalopaswa kusikilizwa kwa uwazi ili jamii yote ijifunze kwa vitendo juu ya maana ya utii wa sheria na namna taifa linavyolinda usalama wake.

Katika maelezo yake, Dkt. Bagonza amesema alitarajia kuwa kesi hiyo ingesikilizwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa uwazi, ingerushwa mubashara na vyombo vya habari, wananchi wangepelekwa kwa makarandinga kushuhudia mwenendo wa kesi hiyo kama somo la uraia.

Hata hivyo, ameonesha mshangao kuwa kesi hiyo imefungwa kwa hoja ya “umuhimu na unyeti” wake.

“Wananchi ndiyo wahusika wakuu wa kulinda usalama wa taifa – kwa nini wasiruhusiwe kujua kinachoendelea?” amehoji Askofu Bagonza.

Katika sehemu ya mwisho ya tafakari yake, Askofu huyo ametoa pole kwa wote waliowahi kuumizwa au kupoteza katika harakati za kutafuta haki, na akaonya: “Giza la kuona haki ikitendeka linaweza kuwa hatari zaidi kwa jamii.”

Kauli hiyo imetafsiriwa na wengi kama wito wa kuimarisha uwazi wa kimahakama, hasa kwa kesi zinazogusa maslahi ya taifa na jamii kwa ujumla.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!