Latest Posts

BABA MZAZI, PAROKO NA WENGINE 7 WADAKWA MAUAJI YA MTOTO ASIMWE MWENYE UALBINO

Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa vya mtoto Albino Asimwe Novart, aliyeuawa wilayani Muleba mkoani Kagera vikiwa vimehifadhiwa katika vifungashio vya plastiki huku watu hao wakitafuta mteja mkoani Kagera.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatano Juni 19, 2024 na Msemaji wa Polisi David Misime, ukamataji huo umefanikiwa kwa kushirikiana na raia baada ya msako mkali kuanzia Mei 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia Juni 19, 2024.

Misime amesema watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja na baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.

“Watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu. Pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga” Ameeleza Misime.

Watuhumiwa wengine waliotajwa na Misime ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwamo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo.

“Aidha waache kudanganyana kwamba kuna utajiri unaopatikana kwa kumiliki viungo vya binadamu mwenye ualbino kwani si kweli kwasababu kama ingekuwa hivyo familia zenye watoto au ndugu wenye ualbino wangekuwa na utajiri mkubwa lakini badala yake tunaona wakiishi maisha ya kawaida kama sisi wengine” Amemalizia Misime.

Wito huu wa polisi unakuja siku moja baada ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusikitishwa na mauaji hayo na kuomba dakika moja ya kutulia kimya kuomboleza kifo chake wakati wa kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam Juni 18- 19, 202

“Nimesikitishwa na kifo cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ wamenyofoa viungo sijapenda na tumuombee kwa Mungu” Alisema Dkt. Samia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!