Latest Posts

BALOZI WA AMANI AINGILIA KATI MIGOGORO YA MGODI WA MSASA, GEITA

Kufuatia hali ya sintofahamu iliyoibuka katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Msasa, uliopo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, ambayo ilipelekea wachimbaji kutawanywa kwa mabomu ya machozi, Balozi wa Amani nchini Tanzania, Mess Chengula, amewataka wachimbaji pamoja na wamiliki wa leseni kuwa watulivu na kuridhika na kile wanachokipata, huku wakiepuka migogoro inayoweza kuondoa amani katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza na mtandao huu, Balozi Mess amesema anatambua jitihada kubwa zinazofanywa na wachimbaji wadogo katika shughuli zao za uchimbaji, hata hivyo amesisitiza umuhimu wa kuwa na subira kwa sasa, akieleza kuwa tayari kamati imeundwa kwa ajili ya kufuatilia na kushughulikia malalamiko yao, yakiwemo madai yanayohusu kodi ambazo kwa kiasi kikubwa wachimbaji hao wamedai zinawabebesha mzigo mkubwa.

Ameongeza kuwa ni vyema wachimbaji kuendelea kuamini mihimili ya dola, hususan vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kutatua changamoto hizo. Aidha, amewataka wamiliki wa leseni kufuata taratibu na makubaliano yaliyowekwa ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa amani na kwa kuzingatia sheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!