Latest Posts

BARAZA LA MADIWANI LATOA SIKU 7 KUHAMISHWA KWA DAMPO LA TAKA

Katika kikao cha robo ya nne ya mwaka wa Serikali 2023/2024 Baraza la madiwani limeitaka Halmashauri ya Tarime mji kupitia kwa Afisa Afya wilaya Erasto Mbunga kuhakikisha pesa iliyotengwa Shilingi milioni 20 inatumika kwa ajili ya kuhamisha ‘dampo’ lililopo kata ya Nyamisangura mtaa wa Mwangaza kwenda kata ya Nkende eneo la magena inaanza kutumika ili kuondoa kero kubwa kwa wananchi.

Akizungumzia hali ya mazingira ya Tarime mji, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote amesema,

“Tusidanganyane katika vikao vyetu hali ya mazingira maeneo mengi ni mbaya Taka zimekuwa nyingi sababu hazizolewi kwa wakati, hivyo ifike hatua Halmashauri itangaze tenda kazi hiyo ifanywe na wengine kuliko kumtegemea Afisa Afya tu na gari lake moja la kuzoa taka huku hali ya mazingira inazidi kuwa mbaya, Baraza tumekubaliana Kwa pamoja tunakupa siku saba (Afisa mazingira Wilaya) dampo la mwangaza lihamishwe pale”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!