Latest Posts

BARAZA LA MADIWANI MUFINDI LAVUNJWA, SERUKAMBA AWATAKA WATUMISHI KUSIMAMIA MAPATO

Baraza hilo limehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Peter Serukamba, ambapo pamoja na mambo mengine, limejadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), likiwa ni sehemu ya utaratibu wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha uwazi katika matumizi ya rasilimali za umma.

Akizungumza katika kufunga baraza hilo, Mkuu wa Mkoa Mhe. Serukamba amewataka watumishi wote wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kwa weledi, wakisimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato na kuyapeleka kwenye miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Amesisitiza kuwa mapato ya ndani ndiyo moyo wa maendeleo ya halmashauri, hivyo hayapaswi kuachwa yasimamiwe ipasavyo.

Akifunga baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Festo Mgina, amesema baraza hilo limekuwa la mafanikio kwakusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuleta tija iliyokusudiwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!