Latest Posts

BASATA MSIWE “CHAWA” NEY WA MITEGO HANA KOSA/ AFANDE SELE AJITOSA SAKATA LA NAY WA MITEGO

Msanii mkongwe wa muziki wa Hiphop hapa nchini anayefahamika kwa jina maarufu la Afande Sele amejitosa kwenye sakata linalohusisha Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na msanii mwenzake wa Hiphop Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la ‘Nay wa Mitego’ anayekabiliwa na mashtaka manne kufuatia wimbo wake wa ‘Nitasema’ aliouachia hivi karibuni
Afande Sele ameieleza Jambo TV, Jumamosi Septemba 28.2024 kuwa hakuna kitu kibaya chochote kilichoimbwa kwenye wimbo huo na kwamba yale aliyoyazungumza Nay wa Mitego kupitia wimbo wa ‘Nitasema’ yanashabihiana na kauli zinazotolewa na viongozi mbalimbali nchini akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ambao kwa nyakati tofauti wamekemea na kueleza masikitiko yao kufuatia uwepo wa vitendo utekaji, mauaji na mmomonyoko wa maadili kwa ujumla wake
Amesema changamoto kubwa iliyoko BASATA ni kwamba wao wamekuwa wakiwaunga mkono na wakati mwingine kufikia kutoa tuzo kwa wasanii wanaoimba nyimbo za kawaida ikiwemo matusi lakini wasanii kama Nay wa Mitego wanapojitokeza hadharani kuimba nyimbo zinazogusa uhalisia wa jamii wamekuwa wakiingia kwenye hekaheka, kusumbuliwa, na wakati mwingine hata kufungiwa
“Kitendo cha BASATA kuanza kumfungia ni muendelezo uleule, kwamba BASATA wao kanuni yao anayefanya vizuri ndio anayefanya vibaya, na anayefanya vibaya ndio anayefanya vizuri, wanaoimba nyimbo hadi za matusi hawana shida na BASATA wanapewa mpaka tuzo lakini wanaoimba vitu vya msingi wanapata shida sana” -Afande Sele
Ametolea mfano yeye binafsi amewahi kuingia kwenye kadhia hiyo pindi alipoachia wimbo ulioitwa ‘Bila Marekani’ ambao amedai kuwa haukuwa na shida yoyote, lakini BASATA na TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) walimuandama licha ya ukweli kwamba wimbo huo uliungwa mkono na hata na Marekani wenyewe, na kwamba yale aliyoimba kwenye wimbo huo kipindi cha nyuma ndio ukweli ambao Dunia ya leo unaushudia
“BASATA wanapaswa kuwa upande wa jamii, kwa sababu hata mmonyoko wa jamii tatizo kubwa ni maadili, na BASATA ni sehemu ya usimamizi wa maadili hayo kwa hiyo wafanye kazi kama watu wa serikali lakini wajuwe wanafanya kazi kwa ajili ya jamii, lakini sasa isivyokuwa bahati wao wamejivika ‘uchawa’ wa moja kwa moja yaani BASATA ni ‘machawa’ ambayo yameshindikana niseme hivyo” -Afande Sele
Ikumbukwe kuwa mashtaka manne (4) anayutuhumiwa msanii Nay wa Mitego na BASATA yanatakiwa kujibiwa kwa mandishi ndani ya siku saba (7) tangu kutolewa kwake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!