Latest Posts

BITEKO ATAKA USHURU WA HUDUMA UFIKE KWA WANANCHI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha fedha zinazotokana na ushuru wa huduma (Service levy) zinaenda moja kwa moja kwenye maeneo ambayo shughuli za uzalishaji zinafanyika.

Biteko ametoa agizo hilo Septemba 10,2024 Mkoani Mtwara kwenye hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji wa eneo la ugunduzi wa gesi la Ntorya lilipo kata ya Nanguruwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara kwa kampuni ya ARA Petroleum Tanzania ambayo itachimba visima viwili vya gesi asilia.

“Wakurugenzi muone wivu watu wenu kule wapate hizo huduma kutokana na service levy wakati tunatafuta fedha za CSR wapate ela ya service levy kwenye maeneo yao,tunataka haya maeneo yabadilike haraka,na hili jambo lianze sasa na kama alianzi sasa.”Amesema Biteko.

Pia amemuagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kabla ya mwezi Disemba,2024 Vitongoji 18 vya kata ya Madimba,vitongoji 13 vya kata ya Msimbati na vitongoji kadhaa vya kata ya Songosongo viwe vimepata umeme na kuahidi kuwa mkoa huo utapata Gridi ya Taifa.

Aidha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amesema wananchi waliopisha mradi wa uchimbaji wa mradi wa visima viwili vya gesi vilivyopo kata ya Nanguruwe teyari serikali imewalipa fidia za kupisha mradi huo kwa asilimia 98.

Ameongeza kuwa asilimia mbili iliyobaki ilibaki kutokana na changamoto za migogoro ya kifamilia ya wananchi wenyewe ambazo ameahidi kutatuliwa haraka.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame amesema visima viwili vimechimbwa katika kitalu hicho katika Ntorya -1 na Ntorya -2 mwaka 20212 na mwaka 2017

Amesema hadi sasa jumla ya futi za ujazo bilioni 1,642 za gesi Asilia zimegunduliwa na kuhakikiwa na leseni hiyo inayotolewa itawezesha Gesi hiyo iliyogunduliwa katika kitalu hicho kuzalishwa na kuwezesha kuongezeka kwa kiasi cha gesi kinachozalishwa nchini.

Mradi huo unategemea kuzalisha kiasi cha kuanzia futi za ujazo milioni 60 kwa siku na kuongezeka hadi kufikia futi za ujazo milioni 140 kwa siku katika kipindi cha miaka mitatu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya ARA ya uendelezaji wa kitalu hicho cha Ntorya Erhan Saygi amesema mradi huo utakamilika mwaka 2025 na utaongeza ajira kwa watanzania kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amesema Mkoa huo umepata umeme kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha kutumia Gesi Asilia cha ‘power plant’ambapo kwa sasa kituo kina mashine 13 zenye uwezo wa kuzalisha megawati 30.4

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!