Latest Posts

BLASS NICOLOUS AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 14

Blass Nicolous Matowo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa na kusomewa shitaka la ulawiti mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Adelina Ngwaya.

Blass anatuhumiwa kumlawiti kijana wake aliyekuwa akifanya kazi katika duka lake na alikuwa akiishi naye nyumba moja.

Baada ya mtoto kulalamika kwa majirani wiki moja iliyopita na wananchii kupata taarifa walikusanyika katika ofisi ya mtaa wa Kitasengwa na taratibu za kumkamata mtuhumiwa na kumkabidhi kwa Jeshi la Polisi zikafanyika.

Hata hivyo mtuhumiwa Blass alikana kosa hilo na kesi yake imeahirishwa mpaka tareh 4 Julai, 2024 na amerudishwa rumande baada ya kukosa mtu wa kumdhamini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!