Latest Posts

BODI YA USHAURI YAAHIDI KUSIMAMIA KWA WELEDI SHUGHULI ZA ADEM

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu Tanzania (ADEM) Dkt. Leonard Akwilapo, amesema, Bodi ya Ushauri ya Wakala iliyozinduliwa rasmi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha inasimamia kwa weledi utekelezaji wa shughuli za Wakala.

Dkt. Akwilapo ameyasema hayo Agosti 02, 2024 mara baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kuzindua rasmi bodi ya ushauri, ADEM Bagamoyo.

Nae Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid Jumanne Maulid akizungumza katika hafla hiyo amesema menejimenti ya ADEM itashirikiana kikamilifu na wajumbe wa vodi kuhakikisha malengo ya taasisi yanafikiwa kwa ufanisi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!