Latest Posts

CAG: KATIBA INASEMA FEDHA ZIPELEKWE MOJA KWA MOJA, ZIMEKWENDA WAPI TRILIONI 1.14?

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/24 imebaini kuwa jumla ya Shilingi trilioni 1.14 zilizokusanywa kupitia tozo mbalimbali na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hazikuwasilishwa kwenye taasisi husika kama ilivyopaswa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, TRA ilikusanya jumla ya Shilingi trilioni 2.59 kwa niaba ya Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), na Mfuko wa Reli, kisha kuhamishia Wizara ya Fedha. Hata hivyo, Wizara ya Fedha ilihamisha kiasi cha Shilingi trilioni 1.44 pekee kwenda mifuko hiyo, na hivyo kubaki salio la Shilingi trilioni 1.14 sawa na asilimia 44 ya fedha zote zilizokusanywa.

CAG ameonya kuwa kitendo hicho kinakiuka Ibara ya 135(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayotaka fedha zilizotengwa kwa matumizi maalumu zipelekwe moja kwa moja kwenye matumizi hayo na si vinginevyo.

Ripoti inabainisha kuwa kuchelewesha au kutopeleka fedha hizo kumeathiri kwa kiasi kikubwa miradi ya maji, barabara, reli na umeme vijijini, huku mifuko husika ikikosa uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

CAG ametoa wito kwa Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa katika mifuko iliyokusudiwa mara moja, ili kuondoa athari za moja kwa moja kwa wananchi na kasi ya maendeleo ya miundombinu nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!