Latest Posts

CHADEMA MBEYA VIJIJINI: WANAOTAKA UBUNGE WAHAME, G55 MNATAKA KUTUVURUGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mbeya Vijijini kimelaani vikali vuguvugu linaloendelea kuenezwa na kundi la G55 ndani ya chama hicho, kikisema kuwa kundi hilo linataka kukwamisha utekelezaji wa Operesheni ya Taifa ya CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Mbeya Vijijini, Getruda Japhet Lengesela, alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa Jambo TV kuhusu mwenendo wa chama na kampeni ya kudai No Reforms, No Election.

Getruda amesema anasikitishwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA wanaotaka kushiriki uchaguzi mkuu ujao licha ya kutokuwepo kwa mazingira rafiki ya kisheria kwa vyama vya upinzani, ikiwemo sheria na taratibu kandamizi za uchaguzi.

Aidha, Getruda ameonesha mashaka na dhamira ya kundi la G55 akisema wengi wao walihusika kuipitisha ajenda ya No Reforms, No Election katika vikao vikuu vya chama, lakini sasa wanapinga misimamo waliyoiunga mkono awali.

Getruda amewataka wanachama wa CHADEMA wanaotaka kwenda kwenye uchaguzi pasipo mabadiliko ya sheria za uchaguzi na bila tume huru, kuondoka na kutafuta vyama vingine vya siasa vinavyokubaliana na mtazamo huo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu wanachama wote wa CHADEMA kukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa ndani ya chama na kuwaunga mkono viongozi waliopo ili kuendeleza harakati za kuleta mabadiliko ya kweli nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!