Latest Posts

CHADEMA WASHITUSHWA NA TAKWIMU ZA TUME HURU YA UCHAGUZI GEITA

 

Na Joel Maduka, Geita

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Viktoria kimeitaka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, kufanya upya makadilio ya takwimu kwa Mkoa wa Geita kutokana na makadilio yaliyotolewa na tume kutokuwa halisi.

 

Makadilio ya takwimu ambayo yalitolewa na Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi ,Jaji Jacobs Mwambegele ,Mkoa huo unatarajia kuandikisha wapiga kura wapya ,299,672.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Geita,Katibu wa kanda ya Viktoria Zacharia Obadi amesema makadilio ya takwimu ambayo yametolewa na tume sio sahihi kutokana na Mkoa huo kuwa na ongezeko kubwa la watu ambao wanaingia na kutoka na wengine wamekuwa wakiingia kwaajili ya shughuli za uchimbaji na kwamba ni vyema kwa tume wakafanya upya makadilio ya watu ambao wanatarajia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura.

“Kwa makadilio haya tunaona kuwa tume itakuwa imewaacha wananchi wengi kutokana na kwamba Mkoa wa Geita ni wawahamiaji wengi ambao kila siku wanaaminia,na jambo jingine ambalo tume inatakiwa kuchukua taadhari ni idadi ya wanafunzi ambao wamemaliza kidato cha nne kuanzia mwaka 2019,2020 ambapo ndio mara ya mwisho tulifanya kazi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura ,tumechukua Shule moja tu mfano ya Buseresere ,Mwaka jana wanafunzi walimaliza kidato cha nne ni 351 ,Shule nyingine tumechukua mfano ni Nyankumbu ambapo Mwaka jana kidato cha nne walimaliza 171 na shule ya Mwisho ni Kalangalala Mwaka jana walimaliza 353 na Katoro walimaliza zaidi ya mia tatu kwa mfano tu hapa Geita shule za serikali 138 ukiangalia wanafunzi waliomaliza kidato cha nne ni wengi na idadi ya takwimu wanazidi”Alisema Zacharia Obadi.

 

Obadi ameongeza kuwa kwa idadi ya wanafunzi tu na wahamiaji inatosha kuifanya tume kupitia upya makadilio yao kwani endapo wakienda na takwimu walizozitoa zinaweza kusababisha watanzania wengi wenye Sifa wakakosa nafasi ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura.

 

“Tuiombe tume warudi tena mezani wachakate upya hizi takwimu za Mkoa wa Geita kama wataendelea nazo kwa siku ambazo wamezitoa zinaweza kusababisha wananchi wengi kuwaacha kwenye daftari la wapiga kura lakini niombe hili tusiwakatishe tamaa watanzania niombe sana tume iongeze vifaa vya uandikishaji na kuongeza siku kutoka siku saba kama itaonekana wameandikisha na watu bado wapo basi waongeze siku hili kila mtanzania hapate haki yake ya kuandikishwa”Alisema Zacharia Obadi.

 

Aidha amewataka wanachama wa Chama hicho pamoja na watanzania kujitokeza kwa wingi kwenda kuandikishwa kwenye Daftari la wapiga kura ambalo ndio litawapa haki ya kuchagua viongozi ambao wanawaitaji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!