Latest Posts

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAANZA UJENZI KAMPASI YA SONGEA

Shilingi Bilioni 18 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi ya Songea ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), katika juhudi za serikali kukuza elimu, biashara na ajira mkoani Ruvuma.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya eneo la ujenzi kwa Mkandarasi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Ahmed Abbas, alisema kuwa ujenzi huo utasaidia kuongeza idadi ya wasomi, kuinua biashara ndani ya mkoa, kukuza sekta binafsi na kuboresha huduma za kijamii kwa ujumla.

 

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Tsh bilioni 18. Hii ni ndoto ya muda mrefu kwa Ruvuma. Kampasi hii itakuza elimu, kuamsha biashara, na kutoa ajira kwa wananchi wengi,” alisema Kanali Abbas.

Aidha, Kanali Abbas alimpongeza Uongozi wa IAA kwa uamuzi wa kizalendo wa kuanzisha kampasi mkoani humo, akisema itautambulisha mkoa kitaifa na kimataifa.

Mbunge Ndumbaro na Prof. Sedoyeka Watia Neno

Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Damasi Ndumbaro, alieleza kuridhishwa kwake na jitihada za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Ruvuma, huku akihimiza wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali kwa vitendo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha IAA, Prof. Eliamani Sedoyeka, alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wananchi wa Ruvuma kwa ushirikiano mkubwa. Alibainisha kuwa kampasi hiyo inalenga kuwa ya kisasa na ya kimataifa.

Jengo hili litakuwa na ukubwa wa ghorofa tano, uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 4500; ndani yake likiwa na madarasa, maktaba, kumbi za mikutano, ofisi na maabara za Kompyuta. Litajengwa kwa muda wa miezi 12 na Mkandarasi China Aero Technology chini ya msimamizi mshauri Y&P Architect (T) Ltd

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!