Latest Posts

DC LINDI AMULIKA MIRADI YA ELIMU; ASISITIZA MUDA, UBORA NA THAMANI YA FEDHA

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ya elimu kwa wakati, huku akizingatia ubora na thamani ya fedha.

Amesema hayo wakati akikagua miradi ya elimu ya sekondari katika Manispaa ya Lindi inayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.5, fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kupitia Mradi wa Sequip III.

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Dr. Jakaya Kikwete katika Kata ya Nangaru, ambayo inagharimu shilingi 560,552,827; ujenzi wa Shule ya Sekondari Hamida Alqassim katika Kata ya Rasbura kwa gharama ya shilingi 560,552,827; na ujenzi wa Shule ya Sekondari Kitomanga katika Kata ya Kitomanga, unaogharimu shilingi 515,000,000.

Katika ziara hiyo, DC Mwanziva amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa ajili ya kuboresha elimu katika Manispaa ya Lindi. Ameahidi kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.

Miradi hiyo ipo katika hatua tofauti za utekelezaji, huku nguvu kubwa ikiwa imeelekezwa katika kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kutoa huduma stahiki.

Katika ziara hiyo ya kikazi, DC Mwanziva aliambatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Bw. Juma Mnwele; Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Manispaa ya Lindi, Bi. Rehema Nahale; na maafisa kutoka Idara ya Elimu Sekondari na Idara ya Ujenzi wa Manispaa ya Lindi. Lengo lilikuwa ni kuweka usimamizi wa pamoja na kuhakikisha matokeo bora ya miradi hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!