Latest Posts

DC LUDIGIJA ATOA MWEZI MMOJA KITUO CHA AFYA KIKUBIJI KUANZA KUTOA HUDUMA

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, Ngw’ilabuzu Ludigija, ametoa mwezi mmoja kwa wasimamizi wa Kituo cha Afya Kikubiji kuhakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wananchi kabla ya Januari 18, 2025.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, DC Ludigija ameeleza kuwa majengo ya maabara na lile la wagonjwa wa nje (OPD) tayari yamekamilika, hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha huduma kwa wananchi.

“Jamani, tusije kulaumiana. Nataka kituo hiki kianze kutoa huduma za nje mara moja kwa sababu majengo haya yameshakamilika. Wananchi wa hapa wamehangaika vya kutosha, sasa ni wakati wao kupata huduma karibu. Rais Samia hataki wananchi waendelee kuhangaika, na ndiyo maana anaendelea kutuletea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama hii,” amesema Ludigija.

Amewaonya wasimamizi kuwa atarudi Januari kukagua utekelezaji wa agizo hilo na kuhakikisha huduma zimeshaanza kutolewa.

Katika ziara hiyo, DC Ludigija pia ametembelea Kituo cha Afya Hungumalwa, ambako vifaa vya upasuaji vilivyokuwa vinakosekana na kuzuia matumizi ya jengo la upasuaji vilikuwa tayari vimewasili. Ameagiza jengo hilo nalo lianze kutoa huduma za upasuaji mara moja.

Wananchi wa Kata za Hungumalwa na Kikubiji wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika sekta ya afya wilayani humo, wakisema miradi hiyo imewapa fursa ya kupata huduma za afya karibu na kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!