Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Mhe. Angelina Marco Lubela, ameendelea na ziara yake ya kutembelea katika vijiji vya Wilaya ya Serengeti kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi moja kwa moja katika maeneo yao ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kusogeza huduma za serikali karibu na wananchi na kuhakikisha changamoto zao zinasikilizwa na kutatuliwa papo hapo
Katika ziara hiyo, Mhe. Angelina anaambatana na baadhi ya wataalam kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo Leo machi 26,2026 amefika katika kijiji cha Kitunguruma kilichopo kata ya Mbalibali, ambapo amesikiliza na kutatua mgogoro wa kifamilia uliokuwa ukiendelea baina ya Mama aitwaye Nyungu Nyisawa na mtoto wake wa kiume aitwaye John King’ita Gecho, mgogoro uliokuwa unahusu umiliki wa nyumba na ardhi.

Sambamba na hayo katika Kijiji cha Machochwe kilichopo kata ya Machochwe, Mhe. Angelina amefanikiwa kurejesha umiliki wa ardhi kwa watoto Ardhi ambayo iliuzwa baada ya baba yao kufariki huku akiagiza aliyekuwa amenunua ardhi hiyo kurejeshewa fedha zake ili akatafute sehemu nyingine ya kuishi.
Aidha Angelina amesisitiza kuwa serikali imejidhatiti kuwatumikia wananchi kwa uadilifu hivyo viongozi ndani ya Wilaya ya Serengeti hawanabudi kutoka maofisini na kuwafuata wananchi kule waliko ili kusikiliza na kutatua kero zao.
