Latest Posts

DC TABORA AVITAKA VYAMA VYA USHIRIKA KUZINGATIA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Deusdedis Katwale ameviasa vyama vya ushirika nchini kuzingatia masuala ya utunzaji wa mazingira katika shughuli zao

Katwale ameyasema hayo Julai 02,2024 wakati akifungua Kongamano la Mazingira katika siku ya pili ya maadhimisho ya wiki ya Ushirika yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Ipuli Mjini Tabora, ambapo amesema pamoja na vyama hivyo kuwa vinafanya kazi nzuri ya kuwaunganisha wanachama na kuwakwamua kiuchumi lakini kumekuwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira katika baadhi ya shughuli zao za uzalishaji ikiwamo kilimo cha tumbaku.

‘’Kwanza niwapongeze wana ushirika kwani mmekuwa mkifanya kazi nzuri sana katika Taifa letu, lakini kuna baadhi yenu mmekuwa mkiharibu mazingira katika shughuli zenu jambo ambalo ni hatari kwa vizazi vya sasa na vijavyo,’’ Amesema DC Katwale.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Mrajisi Uhamasishaji, Consolata Kiluma amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika inahimiza uhifadhi wa mazingira na imekuwa ikifanya kazi pamoja na wadau mbalimbali, hivyo amevitaka vyama vya Ushirika kuendelea na uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadaye.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!