Latest Posts

DED MILLAO AAHIDI KUGHARAMIA MATIBABU YA MWANAFUNZI ABUYASILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma Shaban Millao mara baada ya kupokea barua ya kuhitajika kwa msaada wa mtoto Abuyasili Abdi Iddy mara moja ameacha kazi zote ofisini na kufika katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu ili kufahamu shida na utatuzi wake.

Millao ametoa ahadi ya kugharamia matibabu yote ya mwanafunzi huyo wa darasa la nne ambaye anaongoza  darasani katika shule ya Msingi Bereko iliyopo Kondoa DC lakini pia ametoa ahadi ya kumkatia bima ya afya.

Kwa upande wake Daktari aliyekuwa ameongozana na Mkurugenzi, Dkt. Yusuph Mandi amesema kuwa ugonjwa unaomsumbua mwanafunzi huyo unapaswa kupatiwa matibabu ya haraka katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye kitengo cha mifupa kwani bila ya kufanya hivyo uvimbe huo utasambaa katika vidole vingine.

Aidha Mkuu wa Shule Msaidizi Mwl. Godlove Ulomi ambaye ndiye aliyemuandikia barua ya msaada wa haraka mkurugenzi kuhusu mwanafunzi huyo, amesema kuwa uvimbe huo unaongezeka kwa kasi na kitendo cha Mkurugenzi kuchukua jukumu hilo ni jambo jema na la kuigwa katika jamii.

Sambamba na hayo Mkurugenzi Millao amesema kuwa suala la kusaidia watoto wenye mahitaji maalum ni jambo linalopaswa kupewa kipao mbele kwani hata kiongozi wa nchi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kinara wa jambo hilo kwa kuwasogezea karibu na kuwapatia elimu bora kama ambavyo watoto wengine wanavyopata elimu.

Hayo yamejiri Februari 26, 2025 baada ya Mkurugenzi Millao kupata barua inayohitaji msaada wa haraka kwa mtoto huyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!