Latest Posts

DKT. BINILITH MAHENGE: ELIMU YA UWEKEZAJI INA TIJA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU-

Mwenyekiti wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Binilith Mahenge, amesema kuwa TIC ina jukumu la kutoa elimu ya uwekezaji kwa wadau na wawekezaji nchini kwa lengo la kuwafahamisha fursa na vivutio vilivyopo pale wanapowekeza na kusajili miradi TIC.

Dkt. Mahenge amesema hayo mapema alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya pili ya Kimataifa ya Viwanda, TIMEXPO 2024.

Maonesho haya yameratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa kushirikiana na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

TIC ni miongoni mwa taasisi za serikali zinazoshiriki katika maonesho haya yanayoleta pamoja washiriki kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na wenye viwanda, wazalishaji, wafanyabiashara, wasambazaji, na wajasiriamali.

Maonesho ya TIMEXPO 2024 yameanza tarehe 26 Septemba kwa kufunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, na kutarajiwa kuisha tarehe 2 Oktoba 2024.

Katika maonesho haya, TIC imekuwa ikitoa elimu kuhusu uwekezaji, majukumu na huduma zinazotolewa kwa wazalishaji, pamoja na kueleza umuhimu kwa wazalishaji kusajili miradi yao TIC.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!