Waziri Biteko alitoa kauli hiyo tarehe 13 Septemba 2024, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wakati wa kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa kuwezesha miradi ya nishati safi ya kupikia katika makambi 22 ya JKT kati ya REA na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

“SUMA JKT ni moja ya wakandarasi wanaotupa fahari sisi Wizara ya Nishati. Chini ya uongozi wa Brigedia Jenerali Petro Ngata, miradi yao imekamilika kwa haraka na kwa muda uliopangwa. SUMA JKT wanastahili kupewa miradi mingine mingi kwa sababu usimamizi wa miradi yao umetupa heshima sisi kama Serikali,” alisema Dkt. Biteko.
Aidha, Dkt. Biteko alieleza kuwa serikali imejipanga kupeleka umeme katika vitongoji mbalimbali nchini, na kumtaka Mwenyekiti wa Bodi ya REA pamoja na menejimenti kuhakikisha SUMA JKT wanapewa kipaumbele katika kazi za dharura na za haraka ili kuhakikisha huduma za umeme zinafika kwa wananchi kwa wakati.
