Latest Posts

DKT. BITEKO: TRENI YA UMEME YA SGR NI USHAHIDI WA UMEME WA KUTOSHA NCHINI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema sekta ya Nishati ni wadau muhimu katika maendeleo na kukua kwa usafiri wa treni ya SGR kutokana na treni hiyo kutumia umeme unaozalishwa kutoka Chalinze- Dodoma.

Dkt. Biteko ameyasema hayo mara baada ya kuwasili katika kituo cha treni ya mwendokasi cha Samia akitumia usafiri huo kutoka Dar es Salaam .

Aidha Dkt. Biteko amesema safari za treni za Reli ya Kisasa (SGR) ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

“Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka”, amesema Dkt. Biteko

Katika kuhakikisha umeme unatosheleza Dkt. Biteko amesema Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwepo wa kutosha wakati wote na kuongeza kuwa wizara inasimamia ujenzi wa laini nyingine ya kuutoa umeme kutoka Chalinze kwenda Dodoma kwa laini kubwa zaidi na kutoa umeme kutoka Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kwenda Dodoma baadae Singida, arusha hadi Mwanza.

Kwa mujibu wa Dkt. Biteko, wizara yake inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa upatikanaji wa umeme unakuwa wa uhakika na kuimarika zaidi. Aliweka wazi mipango ya wizara ya Nishati ambayo ni pamoja na ujenzi wa njia kubwa ya umeme kutoka Chalinze kuja Dodoma.

“Tunajenga line nyingine kuleta umeme kwa kuutoa Chalinze kuja Dodoma kwa line kubwa zaidi, tunatumia line hii ya Kilovoti 220 ambayo siyo kubwa sana na tayari tumeshapara mkandarasi kwa ajili ya kutujengea line ya kuuleta umeme kutoka Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere kuja Dodoma,” alisema Dkt. Biteko, akielezea mipango ya upanuzi wa miundombinu ya umeme nchini.

Aidha, amebainisha kuwa uboreshaji wa upatikanaji wa umeme ni muhimu katika kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi nchini. Biteko alisisitiza kuwa uwepo wa umeme wa uhakika umewezesha ujenzi wa viwanda vipya, kongani za viwanda, na biashara zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

“Sasa kuhusu treni hii ambayo tunatumia umeme, ni ushahidi mwingine kwamba nchi yetu ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi,” alisema.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!