Latest Posts

DKT. MWIGULU AKANA MADAI YA TANZANIA KUFILISIKA NA MIRADI YA MAENDELEO KUSUASUA

Na Amani Hamisi Mjege.

Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni inayoeleza kwamba serikali imefilisika kiasi cha kushindwa kulipa madeni kadhaa yalliyosababisha kusuasua kwa Bwawa la Mwalimu Nyerere na migogoro katika kampuni ya Yapi Merkezi inayohusika na ujenzi wa mradi wa reli ya Kisasa (SGR).

Dkt. Mwigulu amekanusha taarifa hiyo kupitia chapisho lake la mitandao mbalimbali ya kijamii la siku ya Ijumaa tarehe 19 Julai 2024 akiwataka Watanzania kupuuza taarifa iliyochapishwa na ukurasa wa Tanzanialeaks katika mtandao wa X zamani Twitter tarehe 18 Julai 2024 ambayo ilieleza kuwa imepata taarifa kutoka Wizara ya Fedha kwamba serikali haina pesa na imeshindwa kulipa madeni yake.

Taarifa hiyo pia iliambatana na picha iliyonaswa katika kioo cha simu yenye ujumbe kutoka kwa mtu anayedaiwa kutoka wizarani ukieleza kuwa serikali imefilisika na miradi mingi kukwama kutokana na makandarasi kutolipwa fedha zao kwa wakati hivyo kupelekea baadhi ya wafanyakazi kuachishwa kazi kwenye miradi hiyo.

“Pale SGR, makandarasi Yapi Merkezi amepunguza sana wafanyakazi. Bwawa la Mwalimu Nyerere limesimama, na miradi mingi ya barabara imekwama. Yaani kwa kifupi ni hakuna fedha serikalini. Kwa hiyo mnapoona ujambazi wa TRA, watu watambue kwamba hakuna pesa. Niko Hazina ila nakuthibitishia kwamba kuna mkadarasi wa barabara wa kigeni tangu Januari 2024 hajalipwa hata senti 5, kazi imesimama, kuna idara inakosa hata pesa” Umeeleza ujumbe huo.

Katika kutolea ufafanuzi wa jambo hilo Dkt. Mwigulu ameeleza kwamba taarifa hiyo ni ‘uongo mtupu’ na ni ya watu ‘walewale’ wenye kuitakia serikali mabaya.

“Serikali haijafilisika, ameandika hatujalipa bwawa – uongo mtupu, Bwawa la Mwl. Nyerere hatudaiwi hata Invoice moja na wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, (Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW)” Ameeleza Dkt. Mwigulu.

Aidha kuhusu madai ya kampuni ya Yapi Merkezi, Dkt. Mwigulu ameeleza kuwa kampuni hiyo ilikuwa na matatizo madogo ambayo yanaendelea kutatuliwa ikiwamo malipo kulipwa.

“Malipo yameendelea kulipwa kwenye sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa fedha” Ameeleza Dkt. Mwigulu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!