Latest Posts

DKT.NCHIMBI AMNADI DKT.SAMIA, KOOLA ALILIA BARABARA

Mgombea Mwenza wa wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Emmanuelil Nchimbi amesema kuwa Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan ametengeneza mazingira mazuri ya upatikanaji wa kipato halali kwa kila mwananchi ili kukuza uchumi wa nchi.

Ametoa kauli hiyo Septemba 13,2025 katika viwanja vya Polisi Himo,Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjaro katika zoezi la kampeni ya kumuombea kura za ushindi kwa Mgombea Urais Dkt Samia Suluhu Hassan,Mgombea Ubunge wa Vunjo Enock Koola pamoja na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Vunjo.

Amesema kuwa kwa watu wanaopenda kupata kipato halali,Dkt.Samia aliagiza mazingira mazuri ya ulipaji wa kodi yawepo na siyo kufunga akaunti za watu badala yake watanzania walipe kodi kwa hiari yao wenyewe.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne Jimbo la Vunjo Vijiji vyote vimefikiwa na umeme huku Wananchi 40,721 wakipata huduma ya maji safi na salama pamoja na uboreshaji wa miundombinu kwani Vunjo inaongoza kwa kuwa na taa za barabarani 503.

Aidha amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo CCM imejidhatiti kuboresha Utalii kwani ilikuwa kwa mwaka mmoja watalii laki laki sita walikuwa wanapokelewa na sasa ni watalii milioni tano wanaingia nchini kila mwaka kutokana na kazi kubwa aliyoifanya Dkt.Samia.

“Mbali na hayo CCM inadhamiria kutoka katika kilimo cha kuvizia mvua hivyo tunaanzisha skimu za umwagiliaji na Vunjo ni miongoni mwa maeneo hayo kutokana na kuwa na mpango wa kufikisha maji safi na salama kwa miaka mitano ijayo kwa wanavunjo kwa asilimia 99″alisema Dkt.Nchimbi

Aidha amesema kuwa kila Wilaya imepewa utaratibu wa kuanzisha viwanda kulingana na malighafi inayopatikana eneo husika ili kuwezesha kuwepo kwa kongani ya viwanda.

“Hayo yote yataenda sambamba na upangaji wa matumizi ya ardhi ili wakulima na wafugahi waweze kuelewa namna ya kufanya shughuli zao halali” alisema Dkt.Nchimbi

Akizungumza mgombea Ubunge Jimbo la Vunjo Enock Koola amesema bado kuna changamoto ya miundombinu ya barabara na upatikanaji wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya milimani na kueleza kuwa endapo wataichagua CCM wataenda kushughulika na changamoto hizo.

“Kwenye suala la miundombinu ya barabara zipo barabara ambazi bado ni changamoto ikiwemo Barabara ya chekereni-Kahe-mabogini, Pofo-Mandaka-kilema na Uchira-Kisomachi, barabara hizi zumesemewa muda mrefu, wananchi mkinichagua, nitashirikiana na serikali kuhakikisha barabara hizi zinajengwa kwa kiwango cha lami.

Ameongeza kuwa “Maji safi na salama pia tunafahamu katika baadhi ya maeneo hususani ukanda wa juu ipo miradi inasuasua lakini wananchi mkitukopesha imani tutakwenda kutekeleza miradi hiyo na kuimaliza changamoto ya maji safi na salama”.

Aidha Koola aliwasilisha ombi kwa mgombea mwenzaa kwa kuomba Jimbo la Vunjo kuwa halmashauri.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!