Latest Posts

DKT. SAMIA AZIFUMUA TAASISI ZINAZOHUSIKA NA MWENDOKASI DAR, ATUMBUA WAWILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wapya kuongoza taasisi zinazohusika na uendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo haraka nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, na kuwasilishwa na Sharifa B. Nyanga, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, leo Oktoba 2, 2025 jijini Arusha, walioteuliwa ni Bw. Said Habibu Tunda, ambaye ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Anachukua nafasi ya Dkt. Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha Bw. Pius Andrew Ng’ingo, ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Anachukua nafasi ya Bw. Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.

Uteuzi huu ni sehemu ya mabadiliko yanayolenga kuimarisha ufanisi wa huduma ya mabasi yaendayo haraka ambayo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!