Latest Posts

DKT. TULIA AHAMASISHA MAMA LISHE NA WANANCHI KUTUMIA NISHATI SAFI

Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, amewahamasisha mama lishe na wananchi kutumia nishati safi ya gesi badala ya kuni na mkaa ili kutunza mazingira na kuokoa muda wa shughuli za kiuchumi.

Akizungumza Septemba 30, 2023, akiwa na wadau wa nishati safi ya gesi kutoka Kampuni ya Oryx, Dkt. Tulia alisema umefika wakati wa kuachana na matumizi ya kuni na mkaa, akisisitiza kwamba gesi ni njia bora na salama.

Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), alifanya mfano kwa kupika chakula kwa gesi katika mgahawa uliopo Mtaa wa Uyole jijini Mbeya, kama sehemu ya kampeni ya kuhamasisha mama lishe na baba lishe kupika kwa nishati safi. Alisema kampeni hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi badala ya nishati zinazochafua mazingira.

Kwa upande wake, Meneja wa Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx, Peter Ndomba, alieleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikisaidia makundi mbalimbali kupata nishati safi ya kupikia. Alisema kuwa, “Tangu kuanza kampeni yetu, tumeshawezesha kutoa mitungi ya gesi na majiko zaidi ya 70,000 kwa mama na baba lishe.”

Ndomba aliongeza kuwa Kampuni ya Oryx imejikita kusaidia kufanikisha ajenda ya Rais Samia Suluhu Hassan, inayolenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ndani ya miaka 10. Alisema, “Tumeungana na Dkt. Tulia, na amekuwa mfano wa kuigwa katika jitihada hizi. Kitendo chake cha kupika kwa gesi ni ishara kubwa kwamba matumizi ya nishati safi yanawezekana.”

Akiendelea, Ndomba alieleza kuwa mama na baba lishe wengi bado wanategemea kuni na mkaa, hali ambayo inaweka afya zao hatarini. “Tunafahamu kuwa Watanzania zaidi ya 33,000 wanafariki kila mwaka kutokana na matumizi ya kuni na mkaa. Kwa kuanzia na kundi la mama lishe, tunaweza kuokoa maisha mengi.”

Ndomba pia aliongeza kuwa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, kampuni ya Oryx imetoa mitungi ya gesi 1,000 kwa mama lishe na baba lishe mkoani. Mbeya kama sehemu ya juhudi zao za kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!