Na Ritha J. Mushi.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema iwapo atashinda urais wa nchi hiyo atawafukuza wageni kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha BBC Swahili Trump amesema hayo wakati akitoa hotuba ya kuthibitisha nia ya chama chake cha Republican katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba katika mkutano wa chama hicho ambao Trump ameuhudhuria katika siku ya nne na ya mwisho mjini Milwaukee.
Pia Trump ameahidi kukamilisha ukuta aliouanzisha utakaotenganisha Marekani na Mexico, ambako mara nyingi huingilia wahamiaji na kwamba hatua ya kwanza atakayoichukua ni kufunga mpaka.
Trump ametumia zaidi ya saa moja kuwasilisha hotuba yake, ambayo ilizungumzwa zaidi badala ya hotuba iliyoandikwa.