Latest Posts

DUWASA WAINGIA MTAANI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Anna George, Dodoma

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Oktoba 8, 2024, imetembelea Mtaa wa Mlimwa C uliopo jijini Dodoma.

Ziara hiyo imelenga kusikiliza kero na maoni ya wananchi na wateja wa eneo hilo, ambapo malalamiko yaliyotolewa yalihusisha changamoto ya kutopata maji kwa wakati pamoja na kuingiziwa bili ilihali hawapati huduma ya maji.

Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa DUWASA, Bi. Lena Mwakisale, ameeleza kuwa usomaji wa mita za maji kwa wateja hufanyika kila mwezi na ni haki ya kila mteja kushirikishwa katika zoezi hilo.

Pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kusoma mita zao mara wanapopokea ujumbe wa bili, ili kuhakikisha bili waliyopewa inalingana na matumizi halisi ya maji.

Bi. Mwakisale amehitimisha kwa kusema kuwa DUWASA inatambua changamoto ya upungufu wa maji katika Mtaa wa Mlimwa C na imefikia hatua nzuri ya kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanaunganishwa kwenye bomba kubwa lililopo maeneo ya Wajenzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!