Kombora la Israel limeipiga Iran, huku milipuko ikisikika katikati mwa nchi. Milipuko ilisikika katika jimbo la kati la Isfahan na safari za ndege zimesitishwa katika miji kadhaa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran. Mkoa wa Isfahan ni nyumbani kwa kituo kikubwa cha anga, eneo kubwa la uzalishaji wa makombora na maeneo kadhaa ya nyuklia. Kisasi hicho cha Israel kinajiri mara baada ya Iran kurusha zaidi ya ndege zisizo na rubani 300 na makombora katika shambulio lake la kwanza kabisa la moja kwa moja dhidi ya Israel lililofanyika Jumamosi usiku tarehe 13 aprili 2024, ambapo Takribani yote yalinaswa na ulinzi wa anga wa Israel kwa msaada kutoka Marekani, Uingereza na washirika wengine. Shambulio hilo la Iran lilikuwa la kulipiza kisasi baada shambulio la Israel lililoua makamanda wakuu wa Iran nchini Syria tarehe 1 Aprili.