Latest Posts

EWURA YAENDESHA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA JOWUTA, DAR ES SALAAM

Ijumaa Desemba 13.2024 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inaendesha mafunzo ya udhibiti wa huduma hizo kwa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA)

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa JOWUTA Suleiman Msuya amesema chama hicho ambacho kina usajil rasmi pamoja na mambo mengine kimeanzishwa kwa lengo la kupigania maslahi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini

Ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wanachama na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini kwa ujumla wake kuhakikisha wanatangiliza nidhamu, weledi na kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya kisheria inayowaongoza ili waweze kiheshimika miongoni mwa wadau

Kuhusu uwepo wa mafunzo/ semina hiyo, Msuya amesema viongozi wa JOWUTA waliona ipo sababu ya msingi kwa EWURA kutoa mafunzo kwa wanachama wa JOWUTA ili kuwajengea uwezo na uwelewa zaidi kuhusu majukumu ya msingi ya mamlaka hiyo, ili kwa pamoja wanahabari hao wawe mabalozi kwa jamii kuhusu kazi zinazofanywa na EWURA na taasisi zake kwa ujumla

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa EWURA Titus Kaguo ametoa pongezi kwa wanachama na viongozi wa JOWUTA kwa kuanzisha chama hicho akiamini kwamba uwepo wake utasadia kwa kiasi kikubwa kushughulikia na kupigania maslahi na changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa vyombo vya habari

Aidha, Msuya ambaye amemuakilisha Mkurugenzi mtendaji wa EWURA Dkt. James A. Mwainyekule katika hafla hiyo amesema ni matarajio yake kuona chama hicho kitasaidia pia kukuza ubora na weledi kwa wanahabari sambamba na kuona wanafuata taratibu za kitaaluma pindi wanapofanya kazi zao

EWURA ina Kanda sita zilizogawanywa kwenye mikoa mbalimbali ambapo kwa mafunzo hayo ya leo yanahusisha wanachama wa JOWUTA wa mkoa wa Dar es Salaam ambao ni sehemu ya Kanda ya Pwani ya EWURA inayohusisha mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara

Katika hilo, imeelezwa kuwa baada ya hapo mafunzo hayo yataendelea kutolewa kwa wanachama wengine wa JOWUTA walioko kwenye mikoa mbalimbali nchini kutokana na ratiba itakayotolewa siku za usoni.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!