Latest Posts

EWURA YATANGAZA PUNGUZO LA BEI ZA MAFUTA: PETROLI, DIZELI NA MAFUTA YA TAA ZASHUKA KWA OKTOBA 2024

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo ya bidhaa za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa hapa nchini zinazoanza kufanya kazi kuanzia leo, Jumatano ya Oktoba 02.2024 saa 06:01 usiku

Taarifa ya EWURA iliyosainiwa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Dkt. James Mwainyekule imefafanua kuwa katika Bandari ya Dar es Salaam mafuta ya Petroli yatauzwa kwa rejareja shilingi 3,011 na jumla shilingi 2,880.15, wakati kwa Bandari ya Tanga Petroli itauzwa kwa rejareja shilingi 3,016 na jumla shilingi 2,884.77 na katika Bandari ya Mtwara Petroli itauzwa kwa rejareja shilingi 3,016 na jumla shilingi 2,884.93

Kwa upande wa mafuta ya Dizeli kwenye Bandari ya Dar es Salaam yatapatikana kwa rejareja shilingi 2,846 na jumla shilingi 2,714.83, Bandari ya Tanga Dizeli itakapatikana kwa rejareja shilingi 2,859 na jumla shilingi 2,728.21 na kwa Bandari ya Mtwara Dizeli itakapatikana kwa rejareja shilingi 2862 na jumla shilingi 2,730.38

Kama hiyo haitoshi, kwa upande wa Mafuta ya Taa yatapatikana kwa rejareja shilingi 2,943 kwa Bandari ya Dar es Salaam na shilingi 2,812.20 kwa jumla, kwa Bandari ya Tanga yatapatikana kwa rejareja shilingi 2,989 na kwa Bandari ya Mtwara yatapatikana kwa rejareja shilingi 3,016

Aidha, EWURA imebainisha kuwa bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa hapa nchini zinazingatia bei ya mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni, ambapo kwa mwezi Oktoba 2024 bei za kikomo za mafuta zilizotolewa zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za soko la Uarabuni za mwezi Septemba 2024, ikilinganishwa na mwezi Agosti 2024 bei zimepungua kwa asilimia 7.42 kwa Petroli, asilimia 9.15 kwa Dizeli na asilimia 8.23 kwa Mafuta ya Taa

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!