Latest Posts

FEZA SCHOOLS YAPIGA HODI KANDA YA ZIWA

Wakati Maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini yakiendelea mkoani Geita, kampuni mbalimbali zimeshiriki katika maonesho hayo, ikiwa ni pamoja na wauzaji wa magari, mitambo, na bidhaa nyingine za migodini. Hata hivyo, mwaka huu ushiriki wa shule binafsi umeleta mvuto wa kipekee, ambapo shule za Waja, Savannah Plains, na Feza zimejitokeza kushiriki.

Miongoni mwa huduma zinazotolewa katika banda la Feza ni pamoja na usahili wa wanafunzi kwa ajili ya kidato cha kwanza kwa mwaka mpya wa masomo wa 2025.

Afisa Mratibu na msaili wa wanafunzi wa Feza, Huzaifa Sizya, ameeleza kuwa Feza imejikita katika kutoa elimu bora yenye viwango vya kimataifa kupitia shule zenye mtaala wa Kimataifa (Feza International) pamoja na mtaala wa kitaifa chini ya NECTA.

Amesisitiza kuwa Feza imeendelea kuongoza katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na sita kwa miaka mingi, ikijivunia rekodi ya kutoa daraja la kwanza kwa wanafunzi wote kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Huzaifa amebainisha kuwa Feza inajiandaa kufungua shule katika Kanda ya Ziwa ili kuwarahisishia wananchi na wazazi huduma za elimu bora karibu na maeneo yao. Hatua hiyo pia ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora, si bora elimu.

Pia Feza imeweka mpango wa kuwasomesha bure wanafunzi wenye uwezo mkubwa darasani, lakini wanakabiliwa na changamoto za kifamilia na hawana uwezo wa kugharamia masomo yao. Kipaumbele kinatolewa kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi, lengo likiwa ni kuandaa madaktari na wahandisi wa baadaye, ambao watasaidia katika kuendeleza taifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!