Latest Posts

Mbunge wa jimbo la Nzega vijijini (CCM) Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema ni wakati muafaka sasa kwa kila raia wa Tanzania kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt

Mbunge wa jimbo la Nzega vijijini (CCM) Dkt. Hamisi Kigwangalla

@HKigwangalla amesema ni wakati muafaka sasa kwa kila raia wa Tanzania kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.

@SuluhuSamia kwa kazi kubwa na ya kipekee aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitatu (3) tangu aingie madarakani Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bungeni jijini Dodoma leo, Aprili 18.2024 Dkt. Kigwangalla amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshika hatamu ya uongozi katika kipindi kigumu (cha kifo cha Rais aliyekuwa madarakani Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) lakini katika kudhihirisha utashi na uwezo wake wa kiuongozi amesimamia nchi na kuiweka katika hali ya amani na utulivu Amesema kwa jimbo la Nzega vijijini pekee ambalo yeye analiwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo kwa sekta ya elimu jimbo hilo limepata shule mpya za sekondari mbili (2) zilizogharimu zaidi ya bilioni 1.3, madarasa mapya yenye thamani ya zaidi ya bilioni mbili (2), mabweni yaliyogharimu zaidi ya bilioni 100 na mabwalo yaliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 200 katika shule mbalimbali Kwa upande wa elimu ya msingi Dkt. Kigwangalla ameeleza kuwa jimbo hilo limepata shule mpya mbili za msingi na shule shikizi zilizogharimu milioni 849, huku kwenye sekta ya afya jimbo hilo likipatiwa vituo vipya vya afya viwili (2) ambavyo ni Inagama na Lusu ambavyo kwa ujumla wake vimekamilika na vimeanza kutoa huduma za awali ikiwemo upasuaji wa dharura, huduma za kumtoa mtoto tumboni, huduma za wagonjwa wa nje (OPD), sambamba na hilo vituo hivyo vikipatiwa watumishi na gari maalumu la wagonjwa (ambulance) mpya iliyopelekwa kwenye kituo cha afya Lusu Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja (1) uliopita Halmashauri ya wilaya ya Nzega ilianzisha mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepeleka bilioni moja (1), na kwamba mpaka sasa baadhi ya majengo yamekamilika, na baadhi ya huduma za nje (OPD) zimeanza kutolewa Katika kufanikisha miradi ya Barabara vijijini, Mbunge huyo ameeleza kuwa hapo awali kabla ya serikali ya awamu ya sita (6) kuingia madarakani Halmashauri nzima ilikuwa ikipokea fedha si zaidi ya milioni 400 kwa mwaka nzima, lakini kwa sasa bajeti ya miradi ya Barabara vijijini imepanda kutoka milioni 600 na ushee hadi kufikia zaidi ya trilioni 4.2, ambapo jimbo la Nzega pekee limepokea bilioni 4 Aidha, Dkt. Kigwangalla amesema kuwa zaidi ya bilioni 23 zimepelekwa jimboni humo kwa ajili ya kufanikisha usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote vya jimbo hilo kupitia REA, ambapo kabla ya serikali ya awamu ya sita (6) kuingia madarakani vijiji vilivyokuwa vimefikiwa na umeme vilikuwa 28 pekee Kuhusu sekta ya maji Dkt. Kigwangalla amedai kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya maajabu makubwa jimboni kwake kwa kuwa awali jimbo zima hakukuwa na sehemu iliyokuwa ikipata maji ya bomba hata moja, lakini kwa sasa zaidi ya asilimia 76 ya wananchi wa jimbo hilo wanachota maji bombani kupitia miradi ya usambazaji maji vijijini iliyogharimu zaidi ya bilioni 19.3 Kufuatia hayo, Mbunge huyo ametoa wito kwa Wabunge wote, wakazi wa jimbo la Nzega vijijini, wanachama wa CCM, na wananchi wote wa Tanzania kwa ujumla wake hususani watumiaji wa mitandaoni ya kijamii kuanzia sasa pindi wanapochapisha andiko au kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii wasisite kuandika hashtags ya ‘nasimaa na Samia’

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!