Latest Posts

FROLA WA GEITA AJIFUNGUA PACHA, AMUUA MMOJA KISA KUEPUKA USUMBUFU

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Flora Mapolu (33) mkazi wa kitongoji cha Mlima Namba 05 kata ya Lwamugasa wilayani Geita kwa tuhuma za mauaji ya mwanaye mwenye umri wa miezi miwili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo ya Julai 26, 2024, mtoto huyo alikuwa mmoja wa pacha aliojifungua mama huyo, na anatuhumiwa kutenda tukio hilo Julai 22, 2024 akiwa kitongoji cha Miyenze wilayani Bukombe ambapo akiwa na watoto wote anadaiwa kumnyonga mtoto mmoja kupunguza usumbufu.

“Julai 24 2024, jeshi la Polisi lilipata taarifa za uwepo wa mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi miwili ambaye aliuwawa kwa kunyongwa shingo na kisha kukatwa viungo vyake.” Ameeleza SACP Jongo.

Kamanda Jongo amesema baada ya kufika eneo la tukio maofisa wa polisi walikuta mwili huo umekatwa mkono wa kulia na mguu wa kulia na kisha mwili wake kutelekezwa njia inayopitia shambani kwenda kisimani.

“Julai 25, 2024 majira ya saa kumi jioni Jeshi la Polisi lilimkamata Flora Mapolu akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Lwamgasa akiwa na mtoto mmoja wa kiume; na kueleza kuwa, Julai 22, 2024 mtoto wa kike alianza kuugua na kitovu chake kilipasuka hivyo akawa mgonjwa sana hali iliyompelekea yeye mwenyewe kumnyonga kwa kipande cha kitenge kisha kumtupa njiani na kuamua kuendelea na safari yake kwa mumewe” Ameeleza SACP Jongo.

Jeshi la Polisi linakamilisha taratibu za kiuchunguzi na Mtuhumiwa Flora Mapolu atafikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilishwa na limewataka wananchi kuacha vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kuwa watoto nao wana haki ya kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!