Latest Posts

GH FOUNDATION YAWAPIKA POLISI, VIONGOZI WA DINI KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA

Taasisi ya GH Foundation imefanikisha mafunzo kwa askari polisi, maafisa ustawi wa jamii na viongozi wa dini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa wadau mbalimbali na kuboresha mifumo katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, yamelenga kuongeza ufanisi katika kushughulikia vitendo vya ukatili kwa kuwajengea uwezo maafisa wa polisi, maafisa wa ustawi wa jamii, na viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyombo vya habari katika kupambana na ukatili wa kijinsia.

Malengo ya warsha hiyo yalikuwa ni kuimarisha uwezo wa wahusika katika kushughulikia kesi za ukatili wa Kijinsia, kuimarisha ushirikiano kati ya sekta mbalimbali, kuongeza ufanisi katika usimamizi wa takwimu na kuhamasisha viongozi wa dini kuwa vinara wa kampeni za kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.

Wataalamu mbalimbali waliwasilisha mada wakiwemo Wakili William Maduhu, ambaye aliwasilisha mada kuhusu sheria za ukatili wa kijinsia na nafasi ya jeshi la polisi katika kupambana na ukatili, Dr.Chris Mauki, aliyezungumzia msaada wa kisaikolojia katika usimamizi wa kesi za ukatili wa kijinsia, Bi.Riziki Lugina, aliyefundisha umuhimu wa ukusanyaji na uchakataji wa takwimu katika kupambana na ukatili wa kijinsia, na Dkt. Katanta Simwanza, aliyefundisha kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kuzuia ukatili.

Warsha hii ni sehemu ya jitihada za taaasisi ya GH Foundation katika kutekeleza afua zake mbili ambazo ni kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, na kupambana na ukatili wa kijinsia ili kukuza usawa na ujumuishaji katika jamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!