Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, kwa kushirikiana na wadau wa elimu, imeandaa mkakati wa kukabiliana na tatizo la wasiojua kusoma na kuandika, hususani kwa watu wazima, ili wawaliweze kutimiza malengo yao.
Afisa Elimu wa Watu Wazima, Mugisha Baravuga, amebainisha hayo katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima ambapo amesema kuwa, hadi sasa, asilimia 79 pekee ya watu katika halmashauri hiyo ndio wanaojua kusoma na kuandika, na malengo ni kufikia asilimia 100.
Wadau wa elimu wamesisitiza kwamba watu wasiojua kusoma na kuandika wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kufikia malengo yao, na wengi wao wanakutana na aibu katika mchakato wa kujifunza.