Latest Posts

HATA VIJIJINI WATU WANAKULA VYAKULA VYA MAFUTA MENGI, SI MIJINI TU- UTAFITI

Mratibu wa Idara ya Mimea na Mazao ya Bustani katika mradi wa kilimo, chakula na lishe (FoodLAND) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Susan Nchimbi amesema kuna haja ya kutoa matokeo ya tafiti hasa za kilimo na chakula zinazopatikana katika miradi mbalimbali kwa wananchi ili wafahamu matokeo yatakayowasaidia kupanga aina ya lishe kwa ajili ya familia zao

Prof. Nchimbi amezungumza hayo mkoani Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya mradi wa kilimo, lishe na chakula (FoodLAND) ambapo amesema kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo kuna utofauti kidogo tu na ambao unaanza kupungua wa aina ya vyakula kati ya wakazi wa mijini na vijijini huku akitanabaisha jinsi wakazi wa vijijini walivyoanza kula vyakula vya mafuta mengi kama watu wa mjini

Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo Prof. Dismas Mwaseba amesema matokeo ya utafiti huo ni mwongozo muhimu wa usaidizi wa upangaji wa lishe bora nchini Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!