Latest Posts

“HATUTAKI RAMLI CHONGANISHI”, TAMESOT YATANGAZA VITA DHIDI YA WAGANGA MATAPELI; POLISI WASHIRIKISHWA

Na Theophilida Felician, Mwanza.

Chama cha Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania (TAMESOT) kimeendesha mafunzo maalum kwa waganga wa mkoani Mwanza, yakilenga kuimarisha taaluma hiyo, kuongeza ufanisi katika utoaji huduma, na kusafisha taswira ya tiba asili nchini.

Akizungumza katika ziara yake mkoani humo, Katibu Mkuu wa TAMESOT, Bw. Lukas Joseph Mlipu, amesema chama hicho kimeamua kuwekeza kwenye elimu ili kuondoa dhana potofu kuwa tiba asili ni kazi ya watu wasio na elimu. Ili kufanikisha hili, TAMESOT imechapisha vitabu vya miongozo, katiba, na kanuni vitakavyosaidia viongozi na wanachama kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu.

Vita Dhidi ya Ramli Chonganishi:

Bw. Mlipu ametoa onyo kali kwa watu wanaojificha kwenye mwamvuli wa tiba asili kufanya ramli chonganishi na kuwaibia wananchi.

“Hatuko tayari kumuona mwanachama wa TAMESOT akishiriki ramli chonganishi. Watu wa namna hii hawana nia njema na tiba asili, badala yake wanaichafua taaluma yetu kwa matukio maovu. Tumeshaanza kushirikiana na Jeshi la Polisi na mamlaka nyingine kuwadhibiti,” alisisitiza Bw. Mlipu.

Ziara ya Mikoa 10 na Mkutano wa Dodoma:

Katibu Mkuu huyo yupo katika ziara ya mikoa 10, ambapo hadi sasa ameshatembelea Mbeya, Shinyanga, Geita, na Mwanza, akielekea mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni:

 

Uongozi Imara: Kuhakikisha kuna uongozi madhubuti kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa.

 

Ushirikiano wa Serikali: Kuwaunganisha waganga na mamlaka za kiserikali ili wafanye kazi kwa uhuru.

Mkutano wa Dodoma: Amewahimiza waganga kujiandaa kwa mkutano mkubwa utakaowakutanisha na Waziri wa Afya jijini Dodoma hivi karibuni.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!