Latest Posts

ILALA YAIVUNJA REKODI: ILANI YA CCM YATEKELEZWA ZAIDI YA ASILIMIA 100 – DC MPOGOLO

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 umefanikishwa kwa zaidi ya asilimia 100 katika Wilaya hiyo, kufuatia kukamilika kwa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Mpogolo aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam, uliolenga kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

“Kasi ya utekelezaji wa miradi imekuwa ya kuridhisha. Kwa hakika Ilani ya CCM 2020–2025 tumeitekeleza kwa zaidi ya asilimia 100. Tumetekeleza miradi ya kimkakati, ikiwemo ya elimu, afya, na uchumi wa wananchi,” alisema Mpogolo.

Elimu Yapewa Kipaumbele

Mpogolo ametaja baadhi ya miradi mikubwa ya elimu kuwa ni ujenzi wa maghorofa nane ya shule za sekondari yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8, pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kitunda Relini kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.6.

Sekta ya Afya Yapata Nguvu Mpya

Katika sekta ya afya, Mpogolo alisema Serikali imejipanga kujenga vituo vya afya kila kata, akitolea mfano wa ujenzi wa zahanati ya kisasa ya Mzinga na ununuzi wa vifaa tiba na dawa muhimu kwa huduma bora kwa wananchi wa Ilala.

Mikopo Isiyo na Riba: Wananchi Wapewa Kipaumbele

Mpogolo pia alieleza kuwa Wilaya ya Ilala imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuinua uchumi wa wananchi bila riba.

“Uwezo wa Halmashauri kwenye makusanyo umeongezeka. Sasa tunapendekeza fedha za maendeleo – hasa kwenye sekta ya barabara – ziongezwe kutoka asilimia 10 hadi 20,” aliongeza Mpogolo.

Viongozi Wengine Waliohudhuria

Mkutano huo maalum ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, pamoja na wakuu wa idara na vitengo, waliopokea kwa furaha taarifa hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!